50 Cent amburuza Drake na Cardi B akiongeza idadi ya tuzo.
Joyce Shedrack
October 16, 2024
Share :
Rapa wa Marekani Curtis “50 Cent” Jackson ameshinda tuzo ya Hustler Bora wa mwaka kwenye tuzo za kifahari za BET Hip Hop 2024 zilizofanyika alfajiri ya leo huko Las Vegas Marekani.
Tuzo hizo hutolewa kila mwaka kutambua mafanikio ya wasanii wa muziki wa Hip Hop na kipengele cha Hustler Bora huangazia wasanii wanaoonyesha bidii, ubunifu, na ufanisi katika muziki na biashara.
50 Cent alikuwa anashindania kipengele hiko pamoja na wasanii wengine kama Cardi B,Drake,Kendrick Lamar,Megan Thee Stallion,Glorrilla na Fat Joe.