Balozi wa Urusi na RC Mtaka Njombe
Sisti Herman
March 12, 2025
Share :
Balozi wa Urusi nchini Tanzania Mhe. Andrey Avetisyan amefanya ziara ya kutembelea mkoa wa Njombe akipokelewa na Mkuu wa mkoa Mhe. Anthony Mtaka.
Pande mbili zilikubaliana kuimarisha ushirikiano katika fani ya kilimo na biashara na kuvutia wafanyabiashara wa Urusi ili watumie fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Njombe.
Baada ya mazungumzo balozi alitembea mashamba na kiwanda cha chai Kibena, kiwanda cha mbao Tanwat na mashamba ya parachichi akithibitisha ubora wa mazao yanayozalishwa mkoani huku.