Cedric Kaze atambulishwa rasmi Sekhukhune United FC.
Joyce Shedrack
June 9, 2026
Share :
Klabu ya Sekhukhune United FC ya nchini Afrika Kusini imemtangaza rasmi Kocha wa zamani wa Yanga na Kaizer Chiefs raia wa Burundi, Cédric Kaze, kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu hiyo.
Kaze anachukua nafasi ya kocha Eric Tinkler aliyeondoka kwenye majukumu yake na amesaini mkataba wa mwaka mmoja, ukiwa na chaguo la kuongezwa kwa miaka miwili zaidi.
Kocha huyo ataendelea kusalia Afrika Kusini baada ya kuwa sehemu ya benchi la ufundi la klabu ya Kaizer Chiefs, ambapo alihudumu kama msaidizi wa kocha na baadae kama kocha mkuu baada ya Nabi kuondoka ndani ya timu.





