pmbet

Chui aua askari, ajeruhi mwanafunzi

Eric Buyanza

September 3, 2025
Share :

Askari wanyamapori afariki dunia huku wengine wanne wamejeruhiwa na chui aliyevamia makazi ya watu ndani ya jiji. 

Tukio hilo limetokea mapema Septemba Mosi, mwaka huu, katika Mtaa wa Iyago, Kata ya Mahina, jijini Mwanza.

Aliyefariki dunia ni Enock Rugaimukamu (33) Askari wa Idara ya Wanayamapori, ambaye alijeruhiwa na mnyama huyo wakati akishirikiana na wenzake kumdhibiti.

Waliojeruhiwa ni Juma Marwa (10), mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Mahina, Mshangi Mkama (45) mkazi wa Mtaa wa Iyago na Gerald Mang’u (39) askari Polisi na mkazi wa Kisesa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Septemba 2, 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amesema mnyama huyo aliripotiwa kuvamia mtaa huo Agosti 30, mwaka huu.

Amesema baada ya jeshi hilo kupokea taarifa hiyo kwa kushirikiana na kikosi cha askari wa wanayamapori wa TAWA, walianza msako na kukuta tayari amejeruhi raia wawili.

"Askari walifanikiwa kumuona mnyama huyo akiwa amejificha kwenye pango na katika jitihada za kumdhibiti mnyama huyo kwa kumfyatulia risasi za moto alitoka pangoni na kuwajeruhi askari hao akiwamo Rugaimukamu aliyejeruhiwa kichwani, mabegani na mgongoni na kumsababishia kifo," amesema Kamanda Mutafungwa.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet