pmbet

Davido asema alimiliki studio ndani kwao bila baba yake kujua.

Joyce Shedrack

November 30, 2024
Share :

Mkali wa Afrobeat kutokea Nigeria David Adeleke maarufu Davido ameweka wazi safari yake ya kimuziki na kusema kuwa aliwahi kuwa na Studio ya siri ndani ya nyumba ya baba yake waliyokuwa wanaishi pasipo baba yake kujua.

Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni msanii huyo amesema alifanikiwa kufanya hivyo kwa sababu nyumba waliyokuwa wanaishi huko kwao Nigeria ilikuwa ina vyumba zaidi ya 20 hivyo haikuwa rahisi baba yake kujua kama ana Studio na watu walikuwa wanaingia kurekodi.

“Nilikuwa na studio ndani ya nyumba na hakujua, nyumba ni kubwa sana ina vyumba kama ishirini na kitu".

 

Davido anasema alilazimika kufanya hivyo kwa sababu ya kuupenda muziki tangu utotoni lakini alishindwa kuweka studio hiyo chumbani kwake kwa sababu baba yake alikuwa na tabia ya kwenda chumbani kwake kila siku akitoka kazini.

Uliwahi kumficha nini baba yako ?

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet