Hamza afanyiwa upasuaji Nchini Morocco.
Joyce Shedrack
December 2, 2025
Share :
Beki wa kati wa klabu ya Simba Abdulrazack Hamza Jana Disemba 1 amefanyiwa upasuaji siku ya jana nchini Morocco katika kliniki ambayo alifanyiwa upasuaji Moussa Camara na sasa anaendelea vizuri.
Hamza ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari mpaka pale atakapo kuwa vizuri kwaajili ya kurejea uwanjani na bado haijajulikana atakaa nje ya uwanja kwa muda gani.
Beki huyo aliumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii wa kariakoo dabi uliochezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 16 mwaka huu.





