pmbet

Kauli ya Hans Rafael kuhusu Mpanzu Yamponza alimwa barua na Simba.

Joyce Shedrack

February 20, 2026
Share :

Kwa mujibu wa mchambuzi wa soka Wilson Oruma klabu ya Simba imeandika barua kwa mchambuzi wa Crown Media Hans Raphael juu ya taarifa alizowahi kuzitoa kuhusu mshambuliaji wa klabu hiyo Ellie Mpanzu.

Suivi : le choix judicieux d'Élie Mpanzu !

Mzee wa Jambia ameorodhesha hoja walizoandika Simba kwenye barua hiyo wakitaka uthibitisho wa kauli za Hans Raphael juu ya Mpanzu au aombe radhi kwa njia ile ile aliyotumia kutoa taarifa hizo.

 

“EXCLUSIVE;Nimeiona Demand Notice Kutoka Simba SC Kwenda Kwa Hans Raphael Kuhusu Elie Mpanzu yenye Kumbukumbu no SSC/CROWN/2026/02/19/01”

"Malalamiko ya Simba SC Kwa Hans Raphael ni Kwamba ametoa taarifa yenye Lengo La Makusudi la
Kuchochea,Kuupotosha Umma na Kuharibu Jina la Simba Sports na Elie Mpanzu Kwa Kusema

1.Elie Mpanzu anaipenda Yanga Kwa dhati Wakati ana Mkataba na Simba SC

2.Elie Mpanzu ameitaarifu SimbaSC Kusudio lake la Kutaka Kuondoka Dirisha Dogo la Usajili la January au Hawezi Kuongeza tena Mkataba

3.Simba SC wana wasi wasi Kuhusu Elie Mpanzu Kutaka Kujiunga na Yanga

“NOTE; Simba SCwamesisitiza Kauli za hapo Juu ni Muendelezo wa Kauli za Kichochezi dhidi ya Simba SC ambazo Hans Raphael amekuwa akizitoa na Kuchapishwa na Kituo cha Crown Media”

"Simba SC wametoa siku mbili Kwa Hans Raphael atoe Ushahidi/Uthibitisho usio na Mashaka (tangible proof) au aombe radhi kwa namna ile ile na kutumia njia ile ile ambayo aliitumia Kutoa hizi taarifa zake"Ameandika @mzeewajambia .

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet