Liverpool yapata pigo mipango ya kumuua Man City yaingia doa.
Joyce Shedrack
November 30, 2024
Share :
Beki wa kati wa klabu ya Liverpool raia wa Ufaransa Ibrahima Konaté atakosekana kwenye mchezo wa kesho wa ligi kuu Uingereza dhidi ya Manchester City kutokana na jeraha alilolipata kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Konate alipata jereha jumatano usiku wakati klabu yake ikiibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya wababe wa Uefa Real Madrid baada ya kugongana na kinda wa Madrid Endrick na kupata jeraha la goti ambalo litamuweka nje wiki 5-6.
Siku ya kesho vijana wa Arne Slot watashuka dimbani kwenye uwanja wa nyumbani majira ya saa 1 usiku kutafuta alama tatu zitakazowafanya kujishindilia kileleni mwa msimamo wa ligi dhidi ya Man City ambayo haijapata matokeo katika michezo sita mfululizo ya mashindano yote.
Hata hivyo Liverpool wataingia kwenye mchezo huo wakiwa na nguvu mpya baada ya urejeo wa beki wao wa kulia Trent Alexander Arnold aliyekuwa nje kwa zaidi ya wiki tatu kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Aston Villa tarehe 9 Novemba.