Marekani yashambulia boti iliyobeba dawa za kulevya
Eric Buyanza
September 3, 2025
Share :
Rais Donald Trump anasema Marekani imeshambulia boti iliyokuwa imebeba dawa za kulevya kusini mwa Karibea, na kuwauwa walanguzi wakubwa 11 wa biashara hiyo.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Trump alisema operesheni ya kuiteketeza boti hiyo iliwalenga wanachama wa genge la Venezuela la 'Tren de Aragua' waliokuwa wakisafirisha mihadarati iliyokuwa ikielekea nchini Marekani.






