Miji ya Pokrovsk na Vovchansk yaangukia mikononi mwa Urusi
Eric Buyanza
December 2, 2025
Share :
Makamanda wa kijeshi wa Urusi wamemwambia Rais Putin jana Jumatatu kwamba vikosi vya nchi hiyo vimeiteka miji ya Pokrovsk na Vovchansk nchini Ukraine.
Taarifa hiyo kwa Putin ilisema vikosi hivyo vinaendelea kusonga mbele kwenye maeneo mengine, jambo ambalo rais huyo alijitapa nalo kuwa mafanikio yatakayowezesha kupata ushindi mkubwa zaidi.
Maafisa wa Ukraine hata hivyo bado hawajathibitisha kwamba maeneo hayo yameangukia mikononi mwa Urusi.






