Mkenya aliyehukumiwa kifo Vietnam kisa dawa za kulevya ashinda rufaa.
Joyce Shedrack
July 31, 2025
Share :
Margaret Macharia Nduta raia wa Kenya mwenye umri wa miaka 37 aliyehukumiwa kifo nchini Vietnam mwezi wa tatu mwaka huu kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya ameepuka adhabu hiyo baada ya kushinda rufaa yake.
Mahakama ya Juu ya Vietnam siku ya leo imetangaza kubadilisha hukumu yake na kumuhukumu kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo jambo ambalo limerejesha matumaini kwa ndugu zake.
Mwanamke huyo alipatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya kilo mbili huko Vietnam na kuhumukiwa adhabu hiyo kabla ya serikali ya Nchi yake kuingilia kati na kumsaidia kukata rufaa ambayo wamefanikiwa kushinda.





