Mnyama kuanza safari kesho ya kuwawinda Nsingizini Hotspurs.
Joyce Shedrack
October 15, 2025
Share :
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amethibitisha kuwa klabu ya Simba inatarajia kuondoka Nchini kesho Alhamisi kueleka Nchini Eswatini kwa ajili ya mchezo wao wa kusaka nafasi ya kuingia hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi kitaondoka kesho saa nne asubuhi kwa ndege ya shirika la ndege Tanzania mpaka Johannesburg Nchini Afrika na baadae kuunganisha ndege nyingine mpaka Nchi hiyo.
Mnyama anatarajia kushuka dimbani Jumapili ya tarehe 19 mwezi huu kukiwasha dhidi ya Nsingizini Hotspurs katika uwanja wa Somhlolo majira ya 10 jioni kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.





