Mwendesha mashtaka ICC asimamishwa kazi kwa tuhuma za ngono
Eric Buyanza
June 9, 2026
Share :

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, ICC, Karim Khan amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma za utovu wa maadili.
Mwaka 2024, mfanyakazi wa karibu na Khan alimtuhumu mwendesha mashtaka huyo kwa unyanyasaji wa kingono ikiwa ni pamoja na kumlazimisha kufanya vitendo hivyo, madai ambayo Khan anakanusha.
Taarifa iliyotolewa na kamati ya utendaji ya ICC imesema hatua ya kumsimamisha kazi Khan inatokana na ushahidi na mapendekezo ya ripoti iliyochunguza madai dhidi yake.
Hata hivyo, chombo hicho kimesema uamuzi wa mwisho juu ya iwapo Khan ataondolewa kabisa kwenye wadhifa huo utafikiwa wakati wa kikao maalumu cha nchi wanachama wa mkataba ulioanzisha mahakama hiyo yenye makao yake mjini The Hague.
Khan amekuwa kwenye wadhifa huo tangu mwaka 2021 na miongoni mwa wengine ametoa waranti za kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na Rais Vladimir Putin wa Urusi.
DW





