Nabi alia na waamuzi ligi ya Sauzi
Sisti Herman
February 2, 2025
Share :
Baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya Orlando Pirates kwenye mchezo wa ligi kuu Afrika kusini, kocha mkuu wa Kaizer Chiefs ameonyesha kukerwa na waamuzi wa ligi hiyo kwa namna wanavyoamua matukio mbalimbali.
"Sitazungumza tena kuhusu aina hii ya waamuzi. Utaona kwenye studio yako ikiwa ilikuwa penalti au la. Nikizungumza, kadi nyekundu. Nikimuuliza kuhusu familia yake, kadi nyekundu. Nikiuliza habari yako, kadi nyekundu." alisema Nabi baada ya mchezo huo.
Kauli hiyo ya Nabi imechochewa na namna ambavyo mwamuzi wa mchezo huo aliwapa Orlando Pirates mkwaju wa penati uliowapa goli la pekee ambapo mwamuzi alitafsiri kuwa kiungo mshambuliaji Rele Mafokeng' alichezewa madhambi kwenye sanduku akishambulia.