pmbet

Onana wa Man Utd aachwa Cameroon

Sisti Herman

December 2, 2025
Share :

 

Andre Onana ameachwa nje ya kikosi cha Cameroon kitakachoshiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) - huku timu hiyo ikiwa katika machafuko baada ya kocha mkuu Marc Brys kutimuliwa kutokana na madai ya "ujanja".

Siku chache baada ya kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Shirikisho la Soka la Cameroon (Fecafoot), Samuel Eto'o na kamati yake ya utendaji walitangaza kufutwa kazi kwa Brys katika taarifa ya kushangaza.

Inaangazia orodha ndefu ya shutuma za "kutofaulu kitaaluma" zinazoelekezwa kwa Brys, ikijumuisha "kuchochea" wachezaji kukaidi Fecafoot.

Raia huyo wa Ubelgiji - aliyeteuliwa na Wizara ya michezo ya Cameroon mwezi Aprili 2024, uamuzi ambao Eto'o alijaribu mara moja kuubadilisha - pia anashutumiwa "kushirikiana kikamilifu na watu wasiojulikana ndani ya Fecafoot".

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet