pmbet

Oussama: Yakoub ana nidhamu sana, atafanikiwa Simba

Sisti Herman

September 3, 2025
Share :

 

Takwimu zinaonyesha kuwa Taifa Stars kwenye jumla ya michezo 10 iliyopita, imeshinda michezo 6, imetoa sare 2 na kupoteza michezo mara 2 pekee, huku kwenye michezo hiyo wakifunga goli 10, ikifungwa goli 5 pekee wakitoka na hatisafi (Clean Sheet) mara 5, hizi ni takwimu bora zaidi kwa timu hii tangu kuanzishwa kwake hasa kiuzuiaji.

 

Kwa karibu mwaka mmoja na nusu sasa, timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imekuwa na mwendelezo mzuri sana wa viwango vya makipa wake licha ya kupitia changamoto ya kubadili makipa mara kwa mara kwasababu mbalimbali ikiwemo wakosa makipa waliokuwa bora zaidi kutokana na majeraha, kwani ndani ya muda huo wamecheza makipa zaidi ya 6 bila athari kubwa.

 

 

Moja ya sababu kuu ya kutoruhusu kufungwa magoli mengi umetokana na ubora wa aina kocha wa makipa aliyepewa jukumu la kuwasimamia makipa wa timu hii, Oussama Hamadane raia wa Algeria ambaye takwimu zinaonyesha wazi kuwa tangu kupewa jukumu hilo mwishoni mwa mwaka 2023, lango la Taifa Stars limekuwa halifungiki kirahisi kama inavyodhaniwa.

 

PMTV Tanzania imefanya mahojiano na kocha huyo wa makipa mwenye leseni ya kiwango A ya ukocha wa makipa kutoka shirikisho la soka barani Asia, tumejadili naye kuhusu uhamisho wa kipa namba 1 wa timu ya taifa Tanzania kwasasa Yakoub Suleiman kutoka JKT Tanzania kwenda Simba Sports Club, fuatilia hapa chini.

 

 

Mwandishi; Yakoub ni kipa wa aina gani?


Oussama: Yakoub ni kipa mweledi, mtiifu, makini, mwenye juhudi zaidi mazoezini anayependa kazi yake na anatoa kila anachostahili kutoa mazoezini na hata zaidi.

 

Mwandishi; Umeona vipi mwanzo wake kuwa kipa wa timu ya Taifa?


Oussama: Ameanza vizuri sana timu ya Taifa, wakati hii akiwa mwanzoni mwa maisha yake ya soka ndiyo wakati ametengeneza nafasi nzuri kwa Taifa, kwasababu ya nidhamu na kusikiliza anayofunzwa.

 

 

Mwandishi; Kama kocha wa timu ya taifa, yapi maoni yako kwa yeye kujiunga kwake na timu ya Simba?

 

Oussama; Kwake ni hatua nzuri na kubwa zaidi, atapata muda wa kupata uzoefu zaidi na kukua kiushindani.

Mwandishi; Akiwa na Simba, unadhani ni vitu gani ataweza kuongeza zaidi na kupata uzoefu ulioutaja?


Oussama: Kucheza timu kama Simba kuva faida unaipata zaidi kuanzia ndani na nje ya uwanja, mfano ndani ya uwanja ushindani wa nafasi utakupa ukomavu zaidi wa kuelewa mbinu na ufundi huku nje ya uwanja ukubwa wa Simba va presha ya kucheza va mashabiki wengi ukikupa ukomavu wa kiakili zaidi.
 


Mwandishi; Kati ya makipa wote uliowahi kuwafundisha, Yakoub umeuona vipi uwezo wake kulinganisha na wengine?


Oussama: Kiukweli ni kipa wa tofauti sana ukilinganisha na wengine, ana ari ya kufanikiwa zaidi ya wote niliowahi kuwafundisha.

 

Mwandishi: Unadhani anaenda kufanikiwa akiwa na uzi wa Simba?


Oussama: Sina shaka, akiwa na timu kama ile, yenye iliyo na mtaji wa wachezaji wenye uwezo mkubwa kiufundi, makocha wenye mbinu bora kama wale, mashabiki wengi vile nabashiri kuwa anaenda kuanza kikosini.
 


Alimaliza hivyo kocha huyo aliyewahi kuwa kocha wa zamani wa makipa wa timu kama Ismailia ya Misri na pia aliwahi kuwa mchezaji wa timu tofauti kwenye nchi za Arabuni kama Saudi Arabia na Algeria.

 

Kocha huyo, Oussama na kipa wake Yakoub wote kwa pamoja kwenye majukumu ya Taifa Stars kwenye michezo ya kuwania kufuzu Kombe la dunia dhidi ya taifa ya Congo Brazaville na ile ya Niger.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet