Saka awa mchezaji anayelipwa zaidi Arsenal
Eric Buyanza
February 20, 2026
Share :

Bukayo Saka amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na Arsenal, kumfanya abaki klabuni hapo hadi 2031.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England, ambaye ana umri wa miaka 24, amefunga mkataba huo na Arsenal, klabu ambayo alijiunga nayo akiwa na umri wa miaka 8.
Saka atakuwa mchezaji wa Arsenal anayelipwa mshahara wa juu zaidi, ambao ni pauni 300,000 kwa wiki sawa na zaidi ya Shilingi Bilioni 1.
Saka amefunga magoli 79 na kutoa asisti 77 katika michezo 297 aliyochezea kwa Arsenal, na kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Arteta.
Aidha ameichezea timu ya taifa ya England mara 48, akifunga magoli 14.





