Simba yamshusha rasmi kocha wa kumnoa Camara na Yakoub Suleiman.
Joyce Shedrack
October 15, 2025
Share :
Klabu ya @simbasctanzania imemtambulisha rasmi Vitomir Vutov kuwa kocha wa magolikipa akiongeza nguvu kwenye benchi la Meneja Mkuu wa klabu hiyo Dimitar Pantev.

Vutov mwenye umri wa miaka 53 raia wa Bulgaria amejiunga na Simba kuwa kocha mpya wa makipa akichukua nafasi ya Wayne Sandilands aliyeondoka na Fadlu Davids.
Kocha huyo amefundisha timu kadhaa Ligi daraja la juu na Kati nchini Bulgaria kama; Spartak Varna, PFC Lokomotiv, FC Lokomotiv Gorna na Litex Lovech.





