pmbet

Singida BS Yajificha Dar kuitafutia makali Flambeau ya Burundi.

Joyce Shedrack

October 15, 2025
Share :

Kikosi cha timu ya Singida BS kimeweka kambi ya siku mbili Jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kwenda Burundi kwa ajili ya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Flambeau De Centre ya nchini humo.

Singida BS imeweka kambi yake jijini hapa na itakuwa ikifanya mazoezi katika Uwanja wa KMC Complex Mwenge na Ijumaa ndio itaanza safari ya kwenda nchini humo.

Akizungumza na PMTV Tanzania Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida BS, Hussein Massanza alithibitisha kikosi chao kuwa Dar es Salaam na kusema mchezo wao watacheza Jumapili Oktoba 19.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet