Skudu na Mgunda wakiwa kwenye uzi wa AS Vita
Sisti Herman
January 9, 2025
Share :
Aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga Mahlase Makudubela "Skudu" raia wa Afrika kusini na mshambuliaji wa klabu ya Mashujaa FC Ismail Mgunda raia wa Tanzania wameonekana wakiwa kwenye uzi wa klabu ya AS Vita ya DR Congo kwenye picha ya pamoja na wachezaji baada mazoezi ya klabu hiyo.
Wachezaji hao wameonekana pamoja na kikosi hicho wakati huu wa dirisha dogo la usajili huku kukiwa na tetesi zinazowataja wachezaji hao kujiunga na AS Vita klabu hiyo ya Kinshasa.