Steve Nyerere amvaa Niffer adai amekosa Nidhamu kwa Waziri Mkuu.
Joyce Shedrack
November 19, 2024
Share :
Mwigizaji na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao Steven Mengele maarufu Steven Nyerere amemvaa mfanyabiashara maarufu Jenifer Jovin Maarufu Niffer kuhusu alichokiandika jana baada ya agizo la Waziri Mkuu kuhusu kukamatwa kwake.
Mwigizaji huyo amesema mfanyabiashara huyo hakutakiwa kujibu chochote kupitia ukurasa wake wa instagram baada ya Waziri Mkuu kuagizwa akamatwe kwa sababu ni kukosa nidhamu kwa kiongozi wa Nchi.
Ikumbukwe,Siku ya jana wakati wa shughuli ya kuaga miili ya watu waliofariki kwenye ajali ya jengo la Kariakoo Novemba 16,alitoa maagizo ya kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo kwa kosa la kuchangisha michango ya maafa hayo bila kibali.
Baada ya Waziri Mkuu kutoa maagizo hayo mfanyabiashara huyo alichapisha ujumbe kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na lengo la kuwaeleza wafuasi wake kuwa yupo salama lakini baada ya muda mfupi aliufuta ujumbe huo.
Hata hivyo,Niffer alitii agizo la Waziri Mkuu siku ya jana na kuripoti katika kituo cha polisi Dodoma akiwa pamoja na majina ya watu waliochangia fedha za maafa kupitia akaunti zake za benki.





