Swiss Guard maafisa waliofunzwa kijeshi kulinda maisha ya Papa
Eric Buyanza
November 12, 2025
Share :
Umewahi kuona picha za Walinzi hawa mitandaoni?
Basi nakusogezea hii,hawa ni walinzi maalum wa kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani (Papa).
Walinzi wa Papa wanajulikana rasmi kama Swiss Guard (Pontifical Swiss Guard) ni kikosi maalum chenye historia ndefu na heshima kubwa ndani ya Kanisa Katoliki na Vatican.
Swiss guard ni maafisa waliofunzwa kijeshi wanaolinda maisha ya Baba Mtakatifu (Pope) na mali zote za Vatican.
Papa akiwa Vatican analindwa na “Swiss Guard” ambao wameanza kuhudumu tangu mwaka 1506 wakati wa Pope Julius II, baada ya kuomba wanajeshi kutoka Uswisi ambao walijulikana kwa uaminifu, nidhamu, na uwezo wa kivita huku wakiwa ni moja kati ya Majeshi makongwe zaidi duniani.
Ili uwe askari wa jeshi hili lazima uwe Mwanaume Mkatoliki mwenye miaka 18 hadi 30 na ambaye haujaoa na uwe raia wa Switzerland uliyepata Mafunzo ya Jeshi.
Mpaka sasa ni zaidi ya miaka 500 ya 'Swiss Guard' wametoa utumishi wao kwa Papa.
Kikosi hiki hakifundishwi tu mafunzo ya kijeshi na ulinzi wa hali juu pekee, bali wanafundishwa pia sheria za kimataifa, utamaduni wa kidiplomasia, na itifaki za ulinzi wa viongozi wakubwa.






