pmbet

Taarifa njema Brazil Neymar Jr anakaribia kuwa fiti kukiwasha.

Joyce Shedrack

June 9, 2026
Share :

Brazil imepokea habari za kutia moyo kuhusu hali ya afya ya Neymar baada ya mshambuliaji huyo kufanyiwa kipimo cha MRI kilichokuwa kimepangwa. 

Brazil Neymar S Neymar JR Photostream Giocatori Di Calcio

Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) limethibitisha kuwa nyota wa Santos anaendelea vizuri katika mchakato wake wa kupona kutokana na jeraha la misuli ya ndama (calf), ingawa timu ya taifa ya Brazil itaendelea kuwa makini kuhusu kurejea kwake wakati ikianza kampeni yake ya Kombe la Dunia.

 

Brazil imepata nafuu ya kisaikolojia baada ya kipimo cha hivi karibuni cha MRI kuonyesha maendeleo mazuri katika kupona kwa Neymar kutokana na jeraha la kiwango cha pili (grade two) kwenye misuli ya ndama wa mguu wa kulia. Jeraha hilo alilipata Mei 17 alipokuwa akiichezea Santos Madaktari wanaamini kuwa mchakato wake wa kupona unaendelea ndani ya muda uliotarajiwa.

 

Licha ya taarifa hiyo nzuri, Brazil haitaki kumharakisha Neymar kurejea uwanjani. Kipaumbele ni kuhakikisha anapona kikamilifu na kurejesha utimamu wake wa mwili kabla ya kurudi kwenye mashindano.

 

Madaktari wa timu ya Taifa ya Brazil wanachukua tahadhari kubwa ili kuepuka tatizo lolote linaloweza kuchelewesha au kuhatarisha ushiriki wa Neymar katika hatua za baadaye za mashindano. Mpango uliopo ni kuongeza taratibu kiwango cha mazoezi yake kabla ya kufikiria kumrudisha kwenye mechi.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet