Unywaji wa bia 1 hadi 2 kwa siku unaongeza kumbukumbu
Eric Buyanza
November 12, 2025
Share :
Utafiti mpya umeonyesha kuwa watu wanaokunywa bia chupa moja hadi mbili kwa siku wana uwezo mzuri zaidi wa kumbukumbu na kufikiri ikilinganishwa na wale wasiokunywa kabisa.
Watafiti wanasema kiasi kidogo cha pombe kinaweza kusaidia kuboresha mzunguko wa damu kwenye ubongo na kupunguza uvimbe wa ndani, jambo linalosaidia kuongeza uwezo wa akili.
Pombe kidogo inaweza kupanua mishipa ya damu (vasodilation), jambo linaloongeza mtiririko wa damu kwenye ubongo.
Pia inaweza kuongeza kemikali kama 'dopamine' na 'serotonin', zinazohusiana na hisia nzuri na motisha.
Hata hivyo, wataalam wanatoa tahadhari kuwa unywaji kupita kiasi unaweza kuondoa faida hizo na kusababisha madhara ya kiafya.






