Wadakwa kwa kutaka kuingia Spain wakijitia kondoo
Eric Buyanza
February 20, 2026
Share :
Polisi nchini Algeria imewakamata wanaume watatu wanaodaiwa kujaribu kuingia Uhispania kwa kujificha kwenye lori la mifugo na kujigeuza kuwa kondoo.
Kulingana na taarifa, maafisa usalama walitilia shaka baadhi ya “wanyama” hao walioonekana wakitembea kwa miguu miwili huku sura zao zikionekana za kibinadamu.
Washukiwa hao, wenye umri wa kati ya miaka 25 na 30, wanaweza kukabiliwa na mashtaka ya udanganyifu wa uhamiaji.






