Wallace Karia ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF.
Joyce Shedrack
March 12, 2025
Share :
Rais wa TFF na CECAFA, Wallace Karia amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya utendaji ya CAF itakayokuwa nchini ya Rais wa CAF, Patrice Motsepe ambae amechaguliwa tena kuwa Rais wa CAF.
Wajumbe wengine ni Samuel Etoo UNIFFAC, Sadi Walid kutoka UNAF, Mustapha Ishola wa WAFU, Kurt Edwin wa WAFU B na Bestine Kazadi.
Wallace Karia ameambatana na Makamu wa Rais wa TFF, Athumani Nyamlani, Katibu wa TFF Wilfred Kidao lakini watanzania wengine ni Salim Abdallah Muhene 'Try Again' Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba lakini pia Rais wa vilabu Africa ACA, Eng Hersi Said.