" Tutaenda kufia uwanjani kwa ajili ya Yanga" - Gamondi
Joyce Shedrack
February 23, 2024
Share :
Meneja wa klabu ya Yanga Walter Harrison amesema kocha Mkuu wa klabu ya Yanga Miguel Gamondi amewataka wachezaji wa Yanga kuhakikisha wanafia uwanjani kuipigania nembo ya Yanga katika mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika timu ya Yanga itakapowakiribisha Cr Belouzdad katika dimba la Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam siku ya kesho majira ya saa 1 jioni.
"Sisi hatuangalii zaidi ni aina gani ya ushindi ambao tutapata kikubwa kinachohitajika ni point tatu lengo letu namba moja ni point tatu Mkuu wa benchi la ufundi kwa maana ya Kocha Mkuu amewaambia wachezaji kinachotakiwa ni kuhakikisha tunaenda kufia uwanjani kwa ajili ya beji ya Yanga " amesema Walter Harrison.
Akizungumzia kikosi cha timu hiyo Harisson amesema mchezaji pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo huo ni Zawadi Mauya ambaye alipata majeraha kwenye mchezo uliopita ila wachezaji wengine wote wapo kamili na wamejiaandaa vizuri kupata ushindi
Hata hivyo hajaacha kugusia msimamo wa kundi lao mpaka sasa katika michuano hiyo akikiri kuwa kundi ni gumu kutokana na ulinganifu wa alama jinsi ulivyo lakini wao wamejipanga kupata ushindi wa alama tatu utaowaweka pazuri kufuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo.