pmbet

18 wapandikizwa betri kwenye moyo Dodoma

Eric Buyanza

February 29, 2024
Share :

Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma imefanya upandikizaji wa betri kwenye moyo ‘pacemakers implantation’ kwa watu watano wiki hii na kufanya idadi yake kufikia watu 18 toka huduma hiyo ianzishwe mwaka 2021.
 

Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo wa BMH, Daktari Bingwa wa Moyo, Happiness Kusima, amesema upandikizaji huo umefanyika kwa watu wenye matatizo ya mfumo wa umeme wa moyo na kusababisha mapigo ya moyo kuwa chini ya kiwango kinachotakiwa kwa mtu wa kawaida ambayo ni 60-100 kwa dakika huku wengi wao huwa ni chini ya 40.
 

Aidha, amesema upandikizaji huo umefanyika kwenye kambi ya Madaktari Bingwa wa Moyo wa BMH kwa kujengewa uwezo na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ya jijini Dar es Salaam.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet