22 wafariki baada ya jengo la shule kuporomoka
Eric Buyanza
July 13, 2024
Share :
Takriban wanafunzi 22 wamefariki dunia baada ya jengo la shule kuanguka wakati wa masomo yakiendelea huko nchini Nigeria.
DW imeripoti kuwa wanafunzi wengine 130 wanapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwenye tukio hilo la kutisha ambapo wengi wa wahanga ni wanafunzi na watumishi wa shule hiyo.
Idadi ya vifo huenda ikaongezeka, kwasababu inaaminika kuwa karibu wanafunzi 200 walikuwa kwenye jengo hilo.
Shughuli za uokoaji bado zinaendelea.