pmbet

50 Bora Spotify Afrika Diamond kumi bora Harmonize nafasi ya 45.

Joyce Shedrack

August 28, 2024
Share :

Staa wa muziki wa bongofleva Diamond Platnumz amekuwa msanii pekee kutoka Tanzania nyimbo yake kuingia kwenye African Heat Playlist ya Spotify ya nyimbo 50 zinazofanya vizuri barani Afrika wiki hii  ngoma yake ya Komasava ikishika nafasi ya  5 kwenye orodha hiyo.

 

Katika orodha hiyo nyimbo 4 za kwanza kwenye playlist hiyo zote ni muziki wa Afrobeat kutoka Nchini Nigeria na  "Komasava" ya Diamond ikifuatia nafasi ya 5 akiwa  msanii pekee kutoka Tanzania aliyeweza kuingia kwenye kumi bora ya playlist hiyo.

Wasanii wengine kutoka Tanzania  kwenye kiwanda cha bongofleva ambao ngoma zao zimeingia kwenye orodha hiyo ni Platform na wimbo wake wa "Ananipenda Remix" ulioshika nafasi ya 12 na Harmonize akishika nafasi ya 45 kupitia ngoma yake ya Disconnect aliomshirikisha Marioo.

 

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet