pmbet

50 Cent atumia picha ya Trump kwenye cover la albam kutoa pole

Eric Buyanza

July 15, 2024
Share :

Huko nchini Marekani, Rapa mkongwe 50 Cent, ametoa pole kwa Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump, baada ya kunusurika kwenye jaribio la kuuawa akiwa kwenye mkutano wa hadhara huko Pennsylvania siku ya jana.

Rapa huyo, ambaye nae pia ameshawahi kunusurika majaribio kadhaa ya kuuawa siku za nyuma, alitoa pole kwa Trump kwa style ya tofauti kwa kubandika picha ya Trump kwenye bango la albamu yake ya ‘Get Rich Or Die Tryin’ wakati wa akiwa kwenye onyesho lake huko Boston siku ya jana.

Wakati akitumbuiza wimbo wake wa ‘Many Men (Wish Death),’ 50 Cent alionyesha bango la albam hiyo huku uso wa Trump ukionekana ndani yake na kuibua shangwe kwa mashabiki.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet