86 wafa maji, huku wengine 185 wakifanikiwa kuogelea hadi ufukweni
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Boti iliyokuwa imebeba abiria 271 imezama kwenye mto karibu na mji mkuu wa Kinshasa nchini Kongo, na kusababisha vifo vya watu 86, Rais Félix Tshisekedi alisema jana Jumatano.
Imetajwa kuwa ajali mbaya ya boti kuwahi kutokea katika siku za karibuni huku wengi wakilalamikia kuzidisha idadi ya abiria huenda ikawa chanzo cha ajali hiyo.
Lakini taarifa iliyomnukuu Rais Tshisekedi ilisema boti hiyo iliyotengenezwa kienyeji ilipinduka Jumatatu jioni katika jimbo la Maï-Ndombe kando ya Mto baada ya kupata hitilafu ya injini.
Abiria 86 walikufa huku wengine 185 wakifanikiwa kuokoa maisha yao baada ya kuogelea mpaka ufukweni.
Itakumbukwa mwezi Februari watu kadhaa walipoteza maisha baada ya boti iliyokuwa imezidisha abiria kuzama nchini humo.