pmbet

Aamka usingizini na kukuta meli iko nje ya nyumba yake

Eric Buyanza

June 4, 2025
Share :

Johan Helberg alikuwa amelala fofofo wakati meli yenye urefu wa mita 135 ilipokosa uelekeo na kuvamia eneo la nyumba yake siku ya Alhamisi ya tarehe 22 May huko kwenye mji wa Trondheim nchini Norway.

Meli hiyo ya mizigo iliyokuwa imebeba makontena ilijikuta ghafla ikiweka nanga nje ya bustani ya Bwana Helberg.

Taarifa zinasema majirani ndio waliokwenda kumuamsha Helberg na kumpa taarifa ya kuwa amevamiwa na mgeni mkubwa sana kwenye bustani yake ndipo alipokimbia kwenda kushuhudia.

Roger Gustafson, kutoka kikosi cha polisi cha eneo hilo, alisema uchunguzi unaendelea ili kujaribu kujua kilichotokea.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet