Aaron anafaa kucheza kama 'James Bond' ajaye - Pierce Brosnan
Eric Buyanza
March 27, 2024
Share :
Muigizaji wa zamani wa filamu za James Bond, Pierce Brosnan hivi majuzi ametoa mtazamo wake juu tetesi za uwezekano wa muigizaji Aaron Taylor-Johnson kuigiza kama James Bond kwenye filamu zijazo.
Akiongea kwenye kipindi cha "The Ray D'Arcy Show," Brosnan hakusita kummwagia sifa Taylor-Johnson huku akisema anastahili kupewa nafasi hiyo.
"Nadhani jamaa na talanta na haiba ya kucheza kama Bond, tena sana tu" alisema Brosnan ambaye kwenye kipindi chake aliigiza kama Bond kwenye filamu 4 ambazo ni "GoldenEye," "Tomorrow Never Dies," "The World Is Not Enough," na "Die Another Day."