Abby Chams ateuliwa kuwa balozi wa UNICEF Tanzania
Sisti Herman
September 29, 2026
Share :

Msanii na mtunzi wa muziki Abigail Chams ameteuliwa kuwa Balozi wa UNICEF Tanzania.
Katika taarifa aliyoichapisha katika ukurasa wake wa Instagram Abby ameandika
”Miaka 6 iliyopita, nilianza safari yangu na UNICEF kama Youth Advocate, nikitumia sauti yangu kutetea afya ya akili, uwezeshaji wa wasichana na haki za watoto.
Today, naanza ukurasa mpya kama Balozi wa Kitaifa wa UNICEF nchini Tanzania#UNICEFNationalAmbassador — jukumu la kuendelea kusimama kwa kila mtoto anayestahili kusikilizwa, kulindwa, kuthaminiwa na kupewa nafasi ya kutimiza ndoto zake.
Na katika mwanzo huu mpya, tumezindua kampeni ya #HaukoSolo
— kukumbushana kuwa it's okay not to be okay éà Kuomba msaada ni UJASIRI. Kuzungumza ni muhimu Hauko peke yako.
Miaka 6 baadaye, purpose yangu bado ni ile ile - For every child.
For every voice. For our future.
@uniceftz OH”
Ameandika Abby





