Abiria mbaroni kwa kukojoa hadharani kwenye korido za ndege
Eric Buyanza
July 12, 2024
Share :
Abiria mmoja aliyefahamika kwa jina la Neil McCarthy aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya American Airlines, alikamatwa baada ya kukojoa hadharani kwenye korido ya ndege hiyo iliyokuwa inaelekea kwenye mji wa New Hampshire nchini Marekani.
Ndege hiyo ililazimika kutua kwa dharura baada ya tukio hilo, na Bwana Neil alikamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuonyesha tabia chafu hadharani.