Abomoa nyumba baada ya mke kumwambia anataka talaka
Eric Buyanza
June 3, 2026
Share :

Huko kwenye Jimbo la Pennsylvania nchini Marekani jamaa mmoja aliyefahamika kwa jina la Eric Pierwsza alichukizwa mno na kitendo cha mkewe kumwambia hamtaki tena huku akisema anaomba talaka yake, kitendo kilichomfanya Bwana Eric kuondoka nyumbani kwa hasira na kwenda kukesha bar akinywa pombe mpaka asubuhi na alivyorudi alipanda kwenye 'excavator' na kuanza kubomoa nyumba yake mwenyewe huku mke na binti zake wawili wakiwa ndani.
Baada ya kuharibu sehemu kubwa ya nyumba hiyo, Eric aliingia ndani akachukua begi lake na kutokomea mjini ambapo baada ya muda alikamatwa na polisi.
Kwa sasa anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya kisheria, ikiwa ni pamoja na kusababisha maafa na kufanya fujo.
Wachunguzi waliwaambia waandishi wa habari kwamba uharibifu wa nyumba hiyo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba sehemu iliyobakia ya nyumba hiyo itahitajika kubomolewa kwa sababu za usalama.





