pmbet

Abu Huzeifa, Kamanda mkuu wa IS auawa nchini Mali

Eric Buyanza

May 1, 2024
Share :

Televisheni ya taifa nchini Mali imeripoti kuuawa kwa kamanda mkuu wa Islamic State ambaye awali kulitangazwa zawadi ya dola milioni 5 za Marekani kwa yeyote atakayetoa taarifa zake.

Abu Huzeifa alikuwa amehusishwa na vamizi kadhaa katika eneo la Sahel, ikiwa na pamoja na shambulio la 2017 ambalo liliua wanajeshi wanne wa Marekani na wanajeshi kadhaa kutoka Niger.

Abu Huzeifa, ambaye pia alijulikana kama 'Higgo', ameuawa na wanajeshi wakiwemo kutoka Mali, Burkina Faso na Niger.

Taarifa hiyo ilisema Huzeifa aliuawa siku ya Jumapili kwenye mji Indelimane.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet