Acheni kunywa pombe kupita kiasi kwani ni kichocheo cha uhalifu
Eric Buyanza
May 16, 2026
Share :

Wananchi wa Kijiji cha Unyamikumbi, Manispaa ya Singida, wametakiwa kuacha tabia ya kunywa pombe kupita kiasi kwani kitendo sio tu ni hatari kwa afya zao bali pia ni kichocheo cha vitendo vya uhalifu hususani shambulio la kudhuru mwili na ubakaji.
Hayo yameelezwa Mei 13, 2026 na Polisi Kata ya Unyamikumbi, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Saidi January huku akisisitiza kuwa kitendo hicho pia hudumuza maendeleo ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.
Aidha, amewakumbusha wananchi hao kutii sheria bila shuruti kwani utii huo wa sheria hupelekea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali na kijamii kufanyika kwa amani na utulivu.
@polisi.tanzania





