"Acheni mauaji ya kimbari Congo" - Lukaku
Sisti Herman
February 16, 2024
Share :
Baada ya kufunga bao la kusawazisha kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Fayernood ya nchini Uholanzi kwenye ligi ndogo ya Ulaya (Europa League), mshambuliaji wa AS Roma ya Italia Romelu Lukaku alishangilia bao hilo kwa kufikisha ujumbe wa kusitishwa kwa mauaji ya kimbari yanayoendelea nchini Congo DR.
Lukaku raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Congo DR baada ya mchezo huo alichapisha picha inayoashiria ujumbe huo huku akiandika ujumbe wa wazi uliosomeka “FREE CONGO DR, STOP GENOCIDE” akimaanisha kusitishwa kwa vita na mauaji ya Kimbari nchini humo.