Achoma moto nyumba ya rafiki yake, kisa kafutwa urafiki kwenye Facebook
Eric Buyanza
July 6, 2024
Share :
Mwaka 2011 mwanadada aliyefahamika kwa jina la Jennifer Christine Harris wa Iowa nchini Marekani, kwa hasira alichoma moto nyumba ya rafiki yake baada ya wawili hao kukosana na baadae rafiki yake huyo kuamua kumfuta urafiki kwenye mtandao wa facebook (kum-unfollow).
Polisi walithibitisha kuwa ni kweli Jennifer alichoma nyumba ya rafiki yake wa zamani Nikki Rasmussen wakati Nikki na mumewe wakiwa wamelala....hata hivyo moto huo haukuleta madhara makubwa baada ya wanandoa kushtuka mapema.