Adakwa akisafirisha nyoka zaidi ya 100 wakiwa kwenye mifuko ya suruali
Eric Buyanza
July 10, 2024
Share :
Mwanaume mmoja wa kichina amekamatwa alipokuwa akijaribu kusafirisha nyoka hai zaidi ya 100 kwenda nchini China akitokea Hong Kong akiwa amewaweka kwenye mifuko ya suruali yake.
Jamaa huyo ambaye jina lake halikutajwa alizuiliwa na maafisa wa forodha alipokuwa akitaka kuvuka mpakani kuingia katika mji Shenzhen.
Baada ya ukaguzi, maofisa hao waligundua mifuko ya suruali yake aliyokuwa amevaa ikiwa imeunganishwa na mifuko sita ya turubai na kufungwa kwa mkanda.
Mara baada ya kufunguliwa, kila mfuko ulikutwa ukiwa na nyoka hai wa maumbo, rangi na ukubwa tofauto tofauti.
Video iliyosambaa mtandaoni inawaonyesha maofisa hao wa forodha wakichungulia ndani ya mifuko ya plastiki iliyojaa nyoka wenye rangi tofauti tofauti.