Adi Yussuf wa Taifa Stars aibukia kwenye Ukocha Leicester City
Sisti Herman
May 10, 2024
Share :
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Adi Yussuf katika kujiandaa na maisha baada ya soka ameamua kujikita kwenye mafunzo ya kozi za ukocha akiwa bado anacheza kwenye ligi za madaraja ya chini nchini Uingereza kunako klabu ya Kattering Town.
Adi Yussuf ambaye mwaka jana mwezi Julai alikamilisha kozi ya UEFA leseni 'B' hivi sasa anashiriki mafunzo ya kozi za UEFA leseni 'A' ambapo anashiriki kwa nadharia na vitendo kwenye timu za vijana za klabu ya Leicester City.
Adi Yussuf mwenye umri wa miaka 31 alikuwa kwenye kizazi cha Stars kilichofuzu na kucheza AFCON 2019 kwa mara ya kwanza baada ya miaka 30 huku pia akiwa mmoja waliosaidia kufuzu AFCON 2023 iliyomalizika nchini IVory Coast hivi karibuni.