Afa baada ya kung'atwa ulimi na mkewe, kisa wivu wa mapenzi
Eric Buyanza
April 3, 2024
Share :
Afisa Kilimo wa Kata ya Neruma katika Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Julius Rubambi (38), ameuawa kwa kuchomwa kisu na kung'atwa ulimi na mkewe kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi huku mkewe Elizabeth Stephen (36) akijeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospitali ya Kibara.
Inadaiwa kuwa chanzo cha ugomvi huo ni mwanaume kumtuhumu mke wake kuwa ameanzisha mahusiano mengine nje ya ndoa.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mara, ACP Salim Morcas, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kuwa tayari mwanamke huyo yupo chini ya ulinzi na uchunguzi unaendelea.
NIPASHE