pmbet

Afanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe wa saratani kwenye njia ya hewa

Eric Buyanza

March 23, 2024
Share :

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila katika kuendelea kutoa huduma za kibingwa nchini imefanya upasuaji wa kuondoa uvimbe wa saratani kwenye njia ya hewa (Total Laryngectomy) kwa kushirikiana na madaktari kutoka MNH Upanga.
 

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Pua, Masikio na Koo, Dkt. Raymond Leiya baada ya kufanyiwa upasuaji huo utamsaidia mgonjwa saratani isisambae katika maeneo mbalimbali ya mwili hivyo kutosababisha madhara zaidi ambapo mgonjwa amewekewa ‘Tracheostomy’ ili kumsaidia aweze kupumua.
 

Dkt. Leiya ameongeza kuwa miongoni mwa visababishi vya saratani ya koo ni uvutaji wa sigara na unywaji wa pombe uliopitiliza.
 

Aidha Dkt Leiya ameishauri jamii kufanya uchunguzi wa mara kwa mara kwa afya zao ili kuweza kubaini kama wanachangamoto mbalimbali za kiafya na kuchukua ili kufanya matibabu mapema na kuepuka madhara.
 

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imekuwa ikitoa matibabu ya kibingwa bobezi kwa matibabu ambayo hayapatikani hapa nchini na hivyo kuwapunguzia wananchi adha ya kwenda nje ya nchi kutafuta huduma hizo, miongoni mwa hudum hizo ni pamoja na huduma ya kupunguza uzito (intragastic balloon), upandikizaji wa figo kwa kuvuna figo kwa kutumia matundu madogo na kutoa uvimbe kwenye ubongo kwa kutumia tundu dogo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet