Afariki akiwa gesti na mpenzi wake
Eric Buyanza
February 28, 2024
Share :
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Mahamudu Mbwana, Mkazi wa Mbezi Madale, jijini Dar es Salaam, amefariki dunia akiwa na mpenzi wake, kwenye nyumba ya kulala wageni (Guest House) iitwayo Another Coast, maeneo ya Mikumbi, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani Lindi.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Lindi, ACP Andrew Ngassa, amesema, baada ya mpenzi wake huyo kuhojiwa na polisi, alisema tarehe 26/2/2024, majira ya saa kumi alfajiri marehemu alianza kuishiwa nguvu na kuanza kukoroma.
Polisi baada ya kupata taarifa walifika eneo la tukio na kuukuta mwili wa marehemu, na walipopekuwa nguo zake walikuta dawa ya kulevya aina ya bangi kwenye mfuko wake wa suruali.
Jeshi la polisi wanamshikilia mpenzi wake huyo kwa mahojiano zaidi.