Afariki baada ya kuumwa na mjusi aliyemfuga
Eric Buyanza
February 23, 2024
Share :
Jamaa mmoja aliyetambulika kwa jina la Christopher Ward, wa Colorado nchini Marekani, amefariki baada ya kuumwa na mjusi mkubwa mwenye sumu 'Gila monster' aliyekuwa akimfuga.
Ward alikuwa akifuga mijusi hiyo miwili na alianza kuugua baada ya kung'atwa mkononi na mmoja wa mijusi hiyo.
Inaelezwa kuwa Ward alianza ghafla kujisikia vibaya, ikafuatia kutapika na kisha akapoteza fahamu na kukimbizwa hospitali ambapo aliwekwa kwenye mashine ya kusaidia kupumua lakini haikuchukua muda alifariki baadae.
Mijusi hiyo ilikuja kuondolewa baadae nyumbani kwake na maafisa wa Idara ya Maliasili.