Afisa mkuu wa Hamas (Ehab Al-Ghussein), auawa na Israel
Eric Buyanza
July 8, 2024
Share :
Afisa mkuu wa utawala wa Hamas alikuwa miongoni mwa watu wanne waliouawa katika shambulio la anga la Israel lililofanyika katika shule moja katika mji wa Gaza, duru za Palestina zinasema.
Afisa mmoja wa eneo hilo ameiambia BBC kwamba Ehab Al-Ghussein aliteuliwa kusimamia maswala ya serikali ya Hamas katika mji wa Gaza na kaskazini mwa Gaza miezi mitatu iliyopita.
Jeshi la Israel linasema kuwa lilifanya shambulio katika eneo hilo kwasababu magaidi walikuwa wakiendesha shughuli zao na kujificha hapo.
Walioshuhudia wamesema shambulio hilo lililenga Shule iliyo karibu na Kanisa la Holy Family, magharibi mwa mji wa Gaza. Idadi kubwa ya watu walikuwa wamejihifadhi katika jengo hilo.
Ehab Al-Ghussein aliwahi kuwa naibu waziri wa kazi katika utawala wa Hamas na kabla ya hapo alikuwa msemaji wa wizara ya mambo ya ndani.
Kifo chake hakichukuliwi kuwa pigo kwa Hamas kijeshi, lakini alichukuliwa kuwa mtu muhimu katika utawala wa Hamas.