Afrika ipo kwenye mikono salama Olimpiki.
Joyce Shedrack
July 31, 2024
Share :
Timu ya Taifa ya Morocco pamoja na Timu ya Taifa ya Misri chini ya umri wa miaka 23 zimetinga nusu fainali ya Mashindano ya Olympic yanayoendelea Paris Nchini Ufaransa.
Misri imefuzu hatua hiyo baada ya kuongoza kundi C kwa alama 9 bila kupoteza mchezo wowote huku Timu ya Taifa ya Morocco imefuzu hatua hiyo kwa kuongoza kundi akikusanya alama 9 pia na kupoteza mchezo mmoja pekee.
Morocco watakutana na Marekani kwenye hatua ya robo fainali na Misri watakipiga dhidi ya Paraguay.
Michezo mingine ya roba fainali ni Argentina dhidi ya Ufaransa na Uhispania dhidi ya Japan.
Mshindi kati ya Morocco na Marekani atakutana na mshindi kati ya Uhispania na Japan na mshindi kati ya Ufaransa na Argentina atakutana na mshindi kati ya Misri na Paraguay.