pmbet

Afrika mashariki yajadili kiwanda cha pamoja cha mafuta

Eric Buyanza

April 24, 2026
Share :

Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinajadili mipango ya kuwa na kiwanda cha pamoja cha kuchakata mafuta katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.

 

Rais wa Kenya William Ruto amesema kuwa nchi za Afrika Mashariki zinajadili mipango ya kuwa na kiwanda cha pamoja cha kuchakata mafuta katika bandari ya Tanga nchini Tanzania. Kiwanda hicho kitaundwa kwa kutumia mfumo wa kiwanda cha Dangote nchini Nigeria.
 

Afrika Mashariki kwa sasa inaagiza bidhaa zake zote za petroli, hasa kutoka Mashariki ya Kati, na kuacha eneo hilo katika hatari ya kuvurugika usambazaji na kupanda kwa bei kama inavyoonekana katika athari za mzozo wa Iran.
 

Ruto aliuambia mkutano kuhusu ufadhili wa miundombinu uliofanyika jijini Nairobi jana kuwa “kiwanda hicho cha pamoja cha Tanga kitanufaisha wote kwa sababu kitachakata mafuta kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Sudan Kusini, na Uganda.”
 

Mfanyabiashara tajiri zaidi barani Afrika Aliko Dangote, ambaye pia alihudhuria mkutano huo, alisema anaweza kutumia muundo wa kiwanda chake cha Nigeria cha kuchakata mapipa 650,000 ya mafuta kwa siku huko Afrika Mashariki, kama serikali katika eneo hilo zitaunga mkono mpango huo.
 

DW

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet